Straika wa kimataifa wa Tanzania ambae anacheza nchini Morocco katika klabu ya Difaa El jadid amefunguka na kuweka wazi kilichoifanya Stars kupata ushindi dhidi ya Botswana
Msuva ambae amejiunga na klabu hiyo katika dirisha kubwa la msimu wa kiangazi ndie aliekua nyota katika mchezo kati ya Tanzania na Botswana kwa kufunga magoli yote mawili yaliyofungwa katika mchezo huo.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo msuva ameongea na waandishi wa habari na kufunga yafuatayo huku akimmwagia sifa Samatta.
“Namshukuru Mungu kwa hatua niliyopiga na nafurahi kurudi nyumbani kulitumikia Taifa langu kwa sababu nimetoka Tanzania na nimepata timu Morocco, kiukweli nje ni nje tukiangalia mfano Samatta ametoka wakati ambao kulikuwa hakuna mchezaji anacheza nje"
“Samatta ametuonesha mfano flani sisi wachezaji wa nyumbani kwa upande wangu nimefurahi Samatta kuonesha njia wengine tunafuata na tumemfuata Samatta kwa wivu wa kimaendeleo, kwa nini yeye anafanya vizuri nje lakini wakati mwingine Samatta huwa anatuambia kila mchezaji una uwezo”>>> Msuva
EmoticonEmoticon