Tuesday, September 26, 2017

KANE WA TOTTENHAM APIGA ZOTE 3 USIKU WA UEFA JANA

Tags




Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane sasa ni moto wa kuotea mbali bila ya kujali ni England tu au Ulaya baada ya jana kupiga hat trick.


Kane ameifunga Spurs mabao matatu ugenini kwa Apoel Nicosia na kushinda kwa mabao 3-0
Mshambuliaji huyo alianza kuzifumania nyavu katika dakika ya 39 mpaka Spurs walivyoenda mapumziko na goli moja.


Kane akaongeza la pili dakika ya 62 na kuongeza la tatu dakika tano baadaye na kitu kilichowashamga kabisa wenyeji ambao walikuwa na ndoto ya kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.


EmoticonEmoticon