Friday, September 1, 2017

LEO MECHI YA KIRAFIKI MAJIMAJI FC VS JKT MALE FC

Tags

MAJIMAJI FC VS JKT MLALE FC

MAJIMAJI STADIUM
4:00 PM
01/09/2017

KIINGILIO. 1000 TU


Leo ijumaa hii ikiwa ni mapumziko ya kazi kutokana na sherehe ya Idd Wanalizombe majimaji fc watashuka ndimbani mechi ya kirafiki na watani wao wa jadi JKT mlale ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza kutoka Songea mjini.

Majimaji fc na JKT malale ni wapinzani wa muda mrefu kutoka na timu hizo kutoka mkoa mmoja wa ruvuma na majimaji walipokuwa wanapambana kupanda daraja walipata wakati mgumu sana walipokutana na JKT MLALE.


kwa sasa majimaji fc iko ligi kuu msimu wa tatu toka ipande daraja na JKT mlale wao bado wakipambana ili nao wapande ligi kuu.

malengo ya michezo ni maandalizi ya ligi kuu kwa Majimaji fc ambao tayari wameshaanza ligi hiyo kwa kucheza ugenini na Mbeya city na wakijikuta wakipoteza michezo huo kwa kufungwa goli moja na sasa wanajiandaa raundi ya pili ugenini tena hukuhuko Mbeya dhidi ya Tanzania prison

Mwalimu msaidizi wa majimaji fc KONDO anaendelea kukisuka kikosi hicho ili kuleta matokeo mazuri kwa michezo inayofuata.


Kwa upande wa JKT MLALE wao pia wanajiandaa na ligi daraja la kwanza inayotaraji kuanza hivi punde mwezi huu wa septemba. Mlale wao wako kundi B na wananafasi kubwa ya kupanda kutoka na  bahati iliyojitokeza mwaka huu kutoka TFF kuwa mwaka huu zitapanda timu 6 kutoka ligi daraja la kwanza na timu 2 tu za ligi kuu zitashuka na kubaki 14 na kuongeza 6 zinazopanda na kuwa jumla ya timu 20 mwakani za ligi kuu.

Hiyo basi katika makundi matatu ya ligi daraja la kwanza kila Lindi lina timu 8 na kila kundi zitapanda timu 2 yaani mshindi wa kwanza na wa pili.

Kocha wa mlale bwana MSABILA anasema uko wakati utafika JKT MLALE itapanda ligi kuu na huo wakati ni msimu huu, timu yetu ni nzuri na imejipanga vizuri na kongwe kwenye ligi hiyo zaidi ya misimu mitano hivyo wanajua changamoto zote kikubwa watupe support wana ruvuma timu yao mwaka huu zitapanda bila shaka.


Michakatoyetu blog tutakuwa live kukujuza matokeo ya michezo huo ndani ya uwanja wa majimaji Leo kuanzia saa kumi jioni

Walio jirani na Songea mjini njooni uwanjani kushuhudia mpamnano huo mkali wa kukata na shoka na kiingilio chako utakuwa umezichangia timu zako za ruvuma ili zifanye vizuri msimu huu na mwakani kuwe na timu mbili za ligi kuu kutoka ruvuma.


Tuonane uwanjani.



EmoticonEmoticon