Saturday, September 2, 2017

MATUIMAINI YA KALLY ONGALA MAJIMAJI NI ZERO

Tags


Kocha Mkuu wa Majimaji, Kally Ongala ameachana na klabu hiyo baada ya kushindwa kumlipa mshahara wake kwa miezi miwili.

Ongala amefanikiwa kuinusuru Majimaji kushuka daraja msimu uliopita kutokana na matokeo mabaya waliyoyapata awali.

Ofisa habari wa klabu hiyo,Onesmo Ndunguru alithibitisha taarifa za kocha huyo kuachia ngazi huku akiwasilisha barua yake ya kujiuzuru wiki iliyopita huku maelezo ya barua yakieleza kudai masilahi yake ya mshahara wa miezi miwili.

Alisema tayari bodi ya klabu hiyo imekaa na kukubaliana na uamuzi aliochukua kocha huyo na nafasi hiyo ikichukuliwa na Habib Kondo.

Ndunguru alisema sababu alizoandika kocha Ongala kwenye barua yake ni kwamba anaidai Majimaji mshahara wa miezi miwili pamoja na matatizo yake ya kifamilia.



‘’Ni kweli Ongala ameachana na Majimaji mara tu baada ya kuiongoza kwa misimu miwili lakini kuondoka kwake siyo kwamba timu itateteleka, bado tupo imara na tutafanya vizuri katika msimu huu wa ligi,’’alisema Ndunguru.

Alisema madai ya kocha huyo kuidai Majimaji mshahara ni jambo ambalo haliwahusu kwani yeye (Ongala) alisaini mkataba na mfadhili wao GSM na siyo Majimaji, lakini kikao cha pili cha bodi kikikaa kitatoa taarifa rasmini.

Ndunguru alisema mkataba wa kocha huyo ulikuwa unamalizika Oktoba mwaka huu lakini kabla ya hapo kocha huyo ameamua kubwaga manyanga.

Alibainisha kuwa kwa sasa timu itakuwa chini ya aliyekuwa kocha msaidizi Habibu Kondo ambaye amepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo iliyoachwa na Ongala.




EmoticonEmoticon