Wednesday, September 20, 2017

AZAM FC HAKUNA KULALA MPERAMPERA.

Tags


Klabu ya Azam FC, leo Jumatano inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers, mchezo utaofanyi katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 19.00 usiku.
Mchezo huo ni muhimu sana kwa ajili ya kuwapa ushindani wachezaji wa timu hiyo, kwani mara ya mwisho kucheza ilikuwa ni Ijumaa iliyopita dhidi ya Kagera Sugar na kushinda bao 1-0.
Hivyo bila mchezo huo wa kirafiki, kikosi hicho kilitarajia kukaa siku takribani tisa bila mchezo wowote, hadi Jumapili hii kitakapochuana na Lipuli ya Iringa kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).


EmoticonEmoticon