Wednesday, September 20, 2017

EMMANUEL MARTINI AREJEA KWENYE UBORA WAKE.

Tags


Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni hii ya Kiungo Mshambuliaji wao, Emmanuel Martin kupona kutokana na majera aliyokua nayo.
Emmanuel Martin aliumia kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Majimaji mchezo ulioisha kwa sare ya goli 1-1, mchezaji huyo anatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya Ndada Fc kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini dare es salaam.
Daktari wa Klabu hiyo Ndugu, Edward Bavu amethibitisha kuwa Martin yuko fiti na amerejea kwenye hali yake, pia mchezaji huyo ameendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wenzake.
“Martin anaendelea vizuri na tayari ameanza mazoezi na wenzake kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Ndanda Jumamosi na kama ni suala la kucheza dhidi ya Ndanda kazi imebaki kwa kocha Mkuu, George Lwandamina lakini mchezaji yupo vizuri,"


EmoticonEmoticon