Monday, September 4, 2017

KOCHA WA BOTSWANA AMKUBALI AISHI MANULA

Tags


Kocha wa Botswana, David Bright, amesifu kiwango kilichoonyeshwa na kipa wa Taifa Stars, Aishi Manula, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa juzi Jumamosi na amesema anatamani kumpeleka Afrika Kusini.

Bright ambaye amewahi kuinoa Santos ya huko Afrika Kusini, alikiri kuwa kiwango cha Manula kilichangia timu yake kushindwa kupata hata bao moja dhidi ya Stars, Botswana ilala 2-0.

Katika mchezo huo, Manula alipangua mashuti matano ya maana ya mastraika wa Botswana ambayo karibu kila mtu aliamini yanakwenda wavuni.

“Ni kipa mzuri sana, anavutia. Amecheza kwa kiwango cha juu sijawahi kuona,” alisema Bright ambaye anaifundisha Botswana kwa mara ya nne sasa.

“Natamani kama ningekuwa bado nafundisha Afrika Kusini, ningekwenda naye kule, amenivutia sana na anastahili pongezi,” aliongeza kocha huyo.


EmoticonEmoticon