Friday, September 1, 2017

DEAL DONE ZA ULAYA JANA HIZI HAPA.

Tags

 


Mamadou Sakho's akitimukia klabu ya Crystal palace kwa ada ya Pauni Milini  26 na Kusaini Mktaba wa miaka Minne

Chelsea's  imemsajili nyota wa Klabu ya Leicester City 'Danny Drinkwater' kwa dau la £35.

Klabu ya Everton imefanikiwa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Croatia airway Nikola Vlasic.

Viasic ametokea katika kikosi cha Hadjuk na amesaini mkataba wa miaka mitano kwa Pauni Million 10.

kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 amejiunga na kikosi cha Kocha Ronald Koeman kinachoendelea kujipanga kufanya vizuri Ligi Kuu England na pia Europa League.l

Klabu ya Liverpool imefanikiwa Kumsajili Winga mwenye kasi Alex Oxlade Chamberlain kutoka Arsenal kwa ada ya Pauni Milioni 35.

Chamberlain amesajiliwa Liverpool ikiwa ni baada ya yeye kukataa kujiunga na Chelsea ambao walifika dau kwa ajili ya kumsaini, lakini hakuwa tayari kutua Darajani hapo, akitoa sababu kuwa Chelsea walitaka kumfanya beki kitu ambacho yeye hakitaki, huku akiwa anataka kutumika kama Kiungo wa kati.


Klabu ya Tottenham Hotspur imefanikiwa kuinasa saini ya beki wa kulia Wa PSG, Serge Aurier, beki huyo anatajwa kuziba pengo lililoachwa na kyle walker aliyetimukia Manchester City 

MuIvory Coast huyo mwenye umri wa miaka 24 amejiunga na Tottenham Hotspur kwa ada ya Pauni Milioni 23 akitokea Klabu ya Paris Saint-Germain ya nchini Ufaransa na kukabidhiwa jezi namba 24.


Leicester City wamemsajili beki Aleksandar Dragovic kwa mkopo kutoka Bayer Leverkusen
Mshambuliaji wa Arsenal Lucas Perez amejiunga tena na Deportivo La Coruna kwa mkopo hadi mwisho wa msimu
Klabu ya Paris Saint-Germain wamekamilisha usajili wa Kylian Mbappe kutoka Monaco, kwa mkopo wakiwa na nafasi ya kumsajili moja kwa moja msimu ujao
Borussia Dortmund wamemsajili kinda wa Manchester City Jaydon Sancho. Manchester City walimpa ruhusa ya kuzungumza na Dortmund, Bayern Munich na Real Madrid peke yake, na hakuruhusiwa kuzungumza na klabu yoyote ya Uingereza.
Klabu ya Lazio imefanikiwa kumsaini Winga Mnero, Mchezaji wa Zamani wa Manchester United Luis Nani akitokea Klabu ya Valencia.
Klabu ya Liverpool imethibitisha kuwa mshambuliaji wake Kinda, Divock Origi amejiunga na Klabu ya Wolfsburg ya Ujeruma kwa Mkopo.
Kinda Wa Buyern Munich Renato Sanches amejiunga na Swansea City kwa Mkopo.
Wilfred Bony amejiunga na klabu yake ya zamani Swansea City kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Man City.
Tottenham Hotspur imemsajili Fernando Llorente kutoka Swansea City kwa mkataba wa miaka miwili.
Chelsea imemsajili beki wa pembeni Davide Zappacosta kutoka Torono kwa pauni milioni 23.

 


EmoticonEmoticon