Wednesday, September 20, 2017

HII HAPA HABARI NJEMA KWA WANA YANGA LEO

Tags


Baada ya kuweka mgomo jana wakidai mishahara ya miezi miwili, hatimaye wachezaji wa Yanga wamerejea kazini leo na kufanya mazoezi.
Mazoezi hayo yamefanyika takribani saa moja kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Chini ya Kocha Mkuu wa Klabu hiyo George Lwandamina, wachezaji hao walifanya mazoezi mepema kabla ya kuondoka na kurejea makwao.
Kabla ya mazoezi wachezaji walifanya kikao cha takribani dakika 17 kabla ya kukubaliana na kuanza mazoezi.
Taarifa zinaeleza, wachezaji bado hawajalipwa na wameahidiwa kuwa suala hilo ndani ya siku mbili tatu litakuwa limefanyiwa kazi na kikubwa wao ni kuendelea na kazi.


EmoticonEmoticon