MKOMBOZI SECONDARY SCHOOL:
HABARI NJEMA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WA KUWAPELEKA SECONDARY.
Mwezi huu wa Tisa vijana wetu darasa la saba wanataraji kumaliza elimu yao ya msingi na kujiandaa na elimu ya sekondari mapema mwezi january, wakati ukiwa kama mzazi ama mlezi wa kijana huyo unawaza mwanao atafanya nini mara baada ya kumaliza mtihani Na pia mwakani atasoma wapi secondary yenye kuleta mafanikio kwa mwanao.
MAJIBU YAKO NI HAYA.
MKOMBOZI SECONDARY SCHOOL, hii ni shule ya private ambayo ni Mpya na ya kisasa ambayo imeandaliwa kwa ajili yako ili mwanao aje kupata elimu iliyo bora kwa weredi mkubwa.
Shule hii inapatikana mkoa wa ruvuma-songea nje kidogo na manispaa kijiji cha KIZUKA ndani ya kata ya MAGAGURA.
Shule hii ina malengo ya kuwasaidia wazazi wawapatie watoto wao elimu bora kwa gharama za kawaida ili hata mzazi mwenye kipato cha chini aweze kumsomesha mwanae.
Shule hii tayari inataraji kuanza rasmi january 2018 na wanafunzi wa kidato cha kwanza.,, ambapo kabla kutakuwa na kozi ya miezi 3 yaani mafunzo ya kujiandaa na kidato cha kwanza PRE FORM ONE kwa masomo yote 9 ya sekondary kuanzia 15/09/2017 hadi 20/12/2017 kwa gharama ndogo sana. Na watakaojiunga na kozi hiyo wananafasi kubwa ya kujiunga kidato cha kwanza mwakani.
Shule inataraji kupokea wanafunzi wa jinsia zote na ni ya BWENI, mabweni yapo ya kutosha.
Walimu ni wa kutosha wenye elimu za juu na uzoefu mkubwa
Mazingira ya Shule ni mazuri kwa kujifunzia kwani pana utulivu wa kutosha na madhari nzuri na shule iko pembeni na makazi ya watu hivyo eneo la shule ninamfanya mtoto awaze masomo tu.
Uso wa mbele wa madarasa
Hapo juu ni madarasa kuna majengo matatu yenye madarasa mawili kila jengo ambayo tayar yanamadawati kila darasa ikiambatana na maktaba

Uso wa nyuma majengo ya madara

Haya ni majengo ya MAABARA jengo moja hapo tayari limekamilika kila kitu, moja ujenzi uko ukikongoni
Hili ni jengo la utawala ambalo mafundi wapo hatua ya mwisho
Hapa ni mwonekano wa pamoja madarasa, Maktaba, maabara na jengo la utawala.

Hili ni BWENI kubwa la wasichana lipo pembeni kidogo na majengo ya Shule. Vitanda pia vipo
EmoticonEmoticon