Thursday, August 31, 2017

MECHI YA KIRAFIKI YA SIMBA YASOGEZWA MBELE HADI JPILI

Tags
                           

klabu ya Simba inawaomba  radhi washibiki wa kandanda nchini kwa kuwa mchezo huo ulitaraji kuchezwa kesho, baina ya Simba na timu ya Jeshi ya Hard Hard Rock toka kisiwani Pemba haitakuwepo,na sasa mchezo huo utachezwa siku ya Jumapili hii ya tarehe 3-9-2017.

Ndugu Msomaji wa michakatoyetu Blog, Mchezo huo umesogezwa mbele kuwapisha Botswana ambao kesho watautumia uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Stars Jumamosi.

MECHI YA KIRAFIKI YA SIMBA YASOGEZWA MBELE HADI JPILI

Tags
                           

klabu ya Simba inawaomba  radhi washibiki wa kandanda nchini kwa kuwa mchezo huo ulitaraji kuchezwa kesho, baina ya Simba na timu ya Jeshi ya Hard Hard Rock toka kisiwani Pemba haitakuwepo,na sasa mchezo huo utachezwa siku ya Jumapili hii ya tarehe 3-9-2017.

Ndugu Msomaji wa michakatoyetu Blog, Mchezo huo umesogezwa mbele kuwapisha Botswana ambao kesho watautumia uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Stars Jumamosi.

MECHI YA KIRAFIKI YA SIMBA YASOGEZWA MBELE HADI JPILI

Tags
                           

klabu ya Simba inawaomba  radhi washibiki wa kandanda nchini kwa kuwa mchezo huo ulitaraji kuchezwa kesho, baina ya Simba na timu ya Jeshi ya Hard Hard Rock toka kisiwani Pemba haitakuwepo,na sasa mchezo huo utachezwa siku ya Jumapili hii ya tarehe 3-9-2017.

Ndugu Msomaji wa michakatoyetu Blog, Mchezo huo umesogezwa mbele kuwapisha Botswana ambao kesho watautumia uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Stars Jumamosi.

MECHI YA KIRAFIKI YA SIMBA YASOGEZWA MBELE HADI JPILI

Tags
                           

klabu ya Simba inawaomba  radhi washibiki wa kandanda nchini kwa kuwa mchezo huo ulitaraji kuchezwa kesho, baina ya Simba na timu ya Jeshi ya Hard Hard Rock toka kisiwani Pemba haitakuwepo,na sasa mchezo huo utachezwa siku ya Jumapili hii ya tarehe 3-9-2017.

Ndugu Msomaji wa michakatoyetu Blog, Mchezo huo umesogezwa mbele kuwapisha Botswana ambao kesho watautumia uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Stars Jumamosi.

MAJIBU YA KAMATI KUHUSU KESI YA CHIRWA NA KASEKE

Tags

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la soka nchini (TFF) imetoa maamuzi ya kuwaruhusu wachezaji Deus Kaseke na Obrey Chirwa kuzitumikia timu zao baada ya kuwakosa na hatia katika tuhuma zilizokuwa zinawakabili.

Hata hivyo Kamati hiyo ilimpata na hatia Saimon Msuva ya kumuangusha mwamuzi wa mpambano wa mwisho la VPL kati ya Yanga dhidi ya Mbao FC.

Kamati imesema Msuva alitakiwa kufungiwa michezo mitatu pamoja na kupewa onyo kali.

Kamati itamwandikia barua la onyo Msuva kwa kuwa alishatumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu wakati wa mashindano ya SportPesa wakati huo akiwa bado ni mchezaji wa Yanga.



SIMBA SC: IDD YA KESHO KUKIPIGA MECHI YA KIRAFIKI NA WAPEMBA

Tags


Klabu ya Simba inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na 
Klabu ya Hard Rock SC, ya Kisiwani Pemba.

Simba kupitia kwa Afisa Habari wake Haji Manara amethibitisha Kuwa na Mechi ya Kirafiki siku ya Ijumaa tarehe 01 September 2017, siku ya (Eid Al Udh -ha) pale Uwanja wa Uhuru majira ya saa 16:00 jioni.


Ndugu Msomaji wa MICHAKATOYETU Blog Katika Mechi hiyi Manara ametaja kuwa kutakuwa na Zawadi mbali mbali, pia Viingilio vimetajwa kwa ajili ya mechi hiyo ambapo VIP itakuwa Tsh:5000/=
Mzunguko itakuwa Tsh:3000/=

AFYA YA CHIRWA YATENGAMAA, ATAANZA LEO MAZOEZI RASMI

Tags

Baada ya kumaliza kujieleza katika kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa anatarajia kuanza mazoezi leo.

Chirwa anarejea katika kikosi cha Yanga baada ya muda wa zaidi ya wiki mbili za kuwa majeruhi.

Chirwa alikuwa aanze mazoezi jana lakini ilishindikana kwa kuwa alitakiwa kujieleza katika kamati ya nidhamu kwa tuhuma za kumsukuma mwamuzi.

Wednesday, August 30, 2017

KOCHA MKUU WA YANGA AMEFIWA NA MSIBA MZITO

Tags

Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, amekumbwa na msiba mzito baada ya baba yake mzazi kufariki.
Lwandamina ambaye amejiunga na Yanga Novemba, mwaka jana, amempoteza baba yake huyo aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kupooza ambapo amefariki usiku wa Jumanne August 29, 2017.
Lwandamina amesema: “Kutokana na msiba huo, natarajia kuondoka leo August 31 kwenda nyumbani Zambia kwa ajili ya mazishi na nikifika ndio tutajua tunazika lini kwani nasubiriwa mimi tu nifike.
“Baba alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kupooza na amefariki Jumanne usiku, nikienda huko nitakaa mpaka kila kitu kimalizike

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 31/08/2017 HAYA HAPA

Tags


















EMMANUEL MARTIN AONGEZWA TIMU YA TAIFA.

Tags

EMMANUEL MARTIN AJUMUISHWA TIMU YA TAIFA STARS KUCHUKUA NAFASI YA SIMON MSUVA

Martin ameitwa kwenye kikosi cha Stars, kuziba pengo la Simon Msuva, ambaye uwezekano wa kuja kutoka Difaal El Jadida ya Morocco ni mdogo
KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga Emmanuel Martin, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachojiandaa kuikabili Botswana, katika mcheo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa Jumamosi hii uwanja wa Uhuru.
Martin ambaye ni mara yake ya kwanza kuitwa timu ya taifa ya Tanzania Bara, alisema hakuamini pendi alipopataa taarifa hizo na anaamini huo ni mwanzo katika safari yake ya mafanikio katika soka.
“Namshukuru kocha kwa kuniona na kulipendekeza jina langu kuwa miongoni mwa wachezaji kwenye kikosi chake naamini nina kubwa ya kufanya ili kufikisha malengo ya timu,”alisema Martin.
Kiungo huyo alisema haikuwa rahisi kwani siku zote alikuwa akiwazia kuichezea timu ya taifa lakini hakupata bahati lakini nafurahi kuona ndoto zake zimetimia.
Amesema atahakikisha anaitumia vizuri nafasi hiyo aliyopewa ili kufanya vizuri na kujitengenezea uhakika wa kuwemo kwenye kikosi hicho kila kinapoitwa tena na kocha Salum Mayanga au yeyote atakayekuwepo.
Martin ameitwa kwenye kikosi cha Stars, kuziba pengo la Simon Msuva, ambaye uwezekano wa kuja kutoka Difaal El Jadida ya Morocco, umekuwa mdogo kutokana na viza yake kuisha muda na sasa uongozi wa timu hiyo upo kwenye mchakato wa kuhakikisha anapatiwa viza ya muda mrefu itakayomwezesha kuingia na kutoka nchini humo.


UTABIRI WA MSUVA KUHUSU BINGWA WA VODACOM MSIMU HUU

Tags
Simon Msuva ana amini kuwa klabu ya Yanga inayo nafasi ya kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo
Klabu ya Yanga itakuwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara nyingine tena kutokana wachezaji wengi kukaa kwa muda mrefu pamoja,  kadhalika na aina ya usajili bora walioufanya msimu huu kwa mujibu wa winga wazamani wa Yanga, Simon Msuva.
Msuva amejiunga na klabu ya Difaa el Jadida ya nchini Morocco, kwa dau linalokadiliwa dola 160,000 lilitumika kumg'oa Yanga.
“Nimefuatilia mechi za mwanzo za ligi ya Tanzania na nimesikia Simba wameanza kwa kushinda 7-0, wakati timu yangu ya zamani ya Yanga ikitoka sare, watu wengi wanasema Simba itakuwa bingwa, lakini binafsi naona Yanga ndiyo yenye nafasi ya kufanya hivyo tena.alisema hivyo wakati akihojiwa na mtandao wa Salehe Jembe.
“Nasema hivyo kwa sababu ukiangalia kweli zote zimefanya usajili wa maana, lakini Yanga ina wachezaji wengi waliokaa pamoja na kuzoeana tofauti na Simba yenye sura nyingi mpya.
Katuka hatua nyingine Msuva amehusifu usajili wa kiungo mkabaji wa Yanga raia wa Congo, Papy Tshishimbi kuwa ni ujio utakao leta tija sababu amekuja tatua tatizo la muda mrefu.
“Lakini pia, Donald Ngoma amerejea vizuri, na yule kiungo mkabaji waliyempata (Papy Tshishimbi), nadhani lile tatizo la siku nyingi limepata mtu sahihi wa kulitibu,” alisema Msuva.

Arsenal yakubali kumwachia Sanchez kwa sharti hili.

Tags
Klabu ya Arsenal iko tayari kumuachia Alexis Sanchez asajiliwe Manchester City.

Lakini sharti lake ni kulipwa pauni milioni 70 na mshambuliaji Raheem Sterling.

Awali, Man City ilikuwa kutoa pauni milioni 50 na Sterling. Lakini Kocha Arsenal Wenger akasema watoe fedha hizo pamoja na mshambuliaji Kun Aguero, Man City nao hawakukubaliana nalo.

Hata hivyo kinachoonekana baada ya muda klabu hizo zitaelewana kabla ya dirisha kufungwa kesho saa sita usiku.

HABARI KUTOKA AZAM FC. SURE BOY NA AGREY MORIS WAONGEZA MKATABA HADI 2019

Tags


NYOTA wawili wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, nahodha msaidizi Aggrey Morris na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ leo wameongeza mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Zoezi la kuingia mikataba hiyo lilisimamiwa na Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Abdulkarim Mohamed ‘Popat’, kwenye Ofisi za timu hiyo Mzizima, zilizopo Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam.
Awali mikataba yao ilitarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu, hivyo kwa kuongeza mikataba mipya, itawafanya wachezaji hao kusalia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2019.
Uongozi wa Azam FC kwa kushirikiana na benchi la ufundi umewaongeza mikataba mipya wachezaji hao, kutokana na viwango vyao bora na mchango mkubwa wanaoendelea kuutoa ndani ya kikosi hicho.
Wawili hao ni wachezaji wakongwe ndani ya kikosi hicho, Sure Boy akianzia kuichezea Azam FC tokea timu hiyo ilipokuwa madaraja ya chini kabla ya kupanda nayo Ligi Kuu mwaka 2008 huku Moris akijiunga na mabingwa hao mwaka 2009 akitokea Mafunzo ya Zanzibar.

USAJILI: TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA

Tags
Kiungo wa kati wa Arsenal Alex Oxlade Chamberlain amekataa uhamisho wa Chelsea baada ya klabu hiyo kukubali dau la £40m.

Oxlade Chamberlain anaamini kwamba Chelsea ilipanga kumtumia kama beki wa kulia huku lengo lake kuu la kutaka kutoka Arsenal likiwa hatua ya kuchezeshwa katikati.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa anataka kuelekea Liverpool,Ombi kutoka Liverpool linatarajiwa kabla ya kukamilika kwa siku ya mwisho ya uhamisho Alhamisi ijapokuwa huenda kitita atakachonunuliwa kikawa chini ya kile ambacho Chelsea wanataka kutoa.

Iwapo hakutakuwa na makubaliano Oxlade Chamberlain yuko tayari kukamilisha mwaka wake wa mwisho wa kandarasi yake msimu huu kabla ya kuondoka kama mchezaji huru msimu ujao.

Arsenal wanataka makubaliano yoyote ya mchezaji huyo kuafikiwa haraka iwezekanavyo.

Oxlade Chamberlain ameanza kila mechi za Arsenal msimu huu ikiwemo kichapo cha siku ya Jumapili cha 4-0 dhidi ya Liverpool, ambapo alitolewa.



Beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, atakataa kujiunga na Arsenal na badala yake anataka kwenda Manchester City. (Daily Mail)

West Brom wanatarajia kumsajili beki wa kati Grzegorz Krychowiak, 27, kutoka Paris Saint-Germain. (Sun)

West Brom pia wanatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Arsenal Kieran Gibbs, 27, katika saa 24 zijazo. (Daily Mirror)

Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, bado ana matumaini ya kwenda Liverpool ingawa Arsenal na Chelsea huenda nazo zikapanda dau katika saa za mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)

Crystal Palace watamuunga mkono meneja wake Frank de Boer kwa kusajili wachezaji watatu wapya. (Daily Star)

Stoke City wanataka kumsajili kiungo wa Manchester City Fabian Delph, 27, na wapo tayari kutoa pauni milioni 12, kwa mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 8 kutoka Aston Villa miaka miwili iliyopita. (Daily Telegraph)

Meneja wa Newcastle United Rafael Benitez yuko tayari kumuuza mshambuliaji wake Dwight Gayle, 26, kwa pauni milioni 18. (Guardian)

Napoli wanataka kumsajili kiungo wa Barcelona Denis Suarez, 23. (Corriere dello Sport)

Winga Adama Traore, 21, anataka kuondoka Middlesbrough kwenda Lille. (Gazette Live)

Divock Origi huenda akaondoka Liverpool na kwenda Tottenham, kwa mujibu wa baba yake. (Sky)

Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Argentina Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 8 na pia bado wanajaribu kumsajili beki wa PSG Serge Aurier, 24, kwa pauni milioni 23. (Guardian)

Liverpool wamekubali kumuuza kiungo Philippe Coutinho, 25, kwenda Barcelona kwa pauni milioni 148. (Yahoo Sports)

Jose Mourinho anataka kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez. (SFR Sport)

Arsenal huenda wakashawishiwa kumuuza Alexis Sanchez, 28, iwapo watapata dau la kuvutia. (BBC Radio 5 live)

Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 30 kutoka Liverpool la kumtaka Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye pia amekataa kwenda Chelsea kwa pauni milioni 40. (Evening Standard)

Raheem Sterling atabakia Manchester City na hatokuwa sehemu ya mkataba wa City kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal. (Sky)

Sergio Aguero huenda akataka kuondoka Manchester City mwezi Januari iwapo Pep Guardiola ataendelea kutomtumia. (Manchester Evening News)

Inter Milan wamepanda dau jipya kumtaka beki wa kati wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25. (Sky Sports)
Tottenham wanafikiria kutopanda dau la kutaka kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, kwa sababu  ni majeruhi kwa sasa. (London Evening Standard)

Arsenal wamepanda dau la kutaka kumsajili winga wa Real Madrid Lucas Vazquez. (Diario Gol)

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa huenda akashangaza wengi na kujiunga na Las Palmas kwa mkopo huku akisubiri kujiunga na Atletico Madrid. (Sun)

Dau la pauni milioni 25 la Chelsea kumtaka Ross Barkley limekataliwa na Everton. (BBC)

Like 

BAADA YA KUPANGUA RATIBA SASA SIMBA RATIBA YAO IKO HIVI

Tags

BAADA YA MABADILIKO HII HAPA RATIBA KAMILI YA SIMBA SC KWA RAUNDI YA KWANZA VPL 2017-2018.

01:Simba vs Ruvu tarehe 26/082017 (7-0)

02:Azam vs Simba tarehe 6/9/2017

03:Simba vs Mwadui tarehe 10/9/2017
                        
04:Mbao vs Simba tarehe 17/9/2017
                          
05:Stend vs Simba tarehe 23/9/2017
                          
06:Simba vs Mtibwa tarehe 1/10/2017
                        
07:Njombe vs Simba tarehe 7/10/2017
                          
08:Simba vs Yanga tarehe 14/10/2017
                        
09:Mbeya Cty vs Simba tarehe 22/10/2017
                        
10:Prisons vs Simba tarehe 28/10/2017
                      
11:Simba vs Lipuli FC tarehe 5/11/2017
                      
12:Ndanda vs Simba tarehe 12/11/2017
                          
13:Simba vs Singida Utd tarehe 19/11/2017
                    
14:Kagera Sugar vs Simba tarehe 16/12/2017
                        
15:Simba vs Majimaji tarehe 24/12/2017

MTOTO AMFANYA BABA AHAMIE NA KUISHABIKIA SIMBA SC

Tags



Baba mzazi wa mtoto Mwamvita Abdulilah aliyepewa msaada wa matibabu wa Sh 2 milioni na klabu ya Simba katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ameamua kuhama kuishabikia Yanga na kujiunga miamba hiyo ya Msimbazi.

Mwamvita aliyelazwa hospitalini hapo kwa zaidi ya miezi miwili akisubiri upasuaji, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kushindwa kupumua vizuri kutokana na kuwa na tundu kwenye moyo amepona na anatarajia kuruhusiwa muda wowote kuanzia sasa.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Abdulilah Bakari alisema amehangaika na mtoto huyo kwa takribani miaka mitatu na hivi sasa nashukuru Mungu kwani amepona baada ya kupatiwa matibabu.

"Nashukuru sana kwa dhati Simba, mimi nilikuwa Yanga damu damu, lakini kutokana na kile ambacho Simba wamenifanyia kutoa Sh2 milioni kumtibia mwanangu nimehama rasmi na sasa nimehamia Simba mimi na familia yangu," alisema Abdulilah.

Naye mtoto Mwamvita alisema anashukuru wanasimba wote kwa kujitoa kuokoa maisha yake, "sasa nitaweza kurudi masomoni nashukuru kwa nafasi hii waliyonipa naomba Mungu awaongezee walipopunguza."

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alielezea Simba News kuwa baada ya kupatiwa fedha za matibabu za Mtoto Mwamvita, walimfanyia upasuaji Agosti 24 mwaka huu.

Alisema upasuaji huo ulifuatia baada ya viongozi na wachezaji wa Simba kutembelea taasisi hiyo Agosti 7 mwaka huu katika maadhimisho ya Simba Day na kukutana na Mwamvita ambaye alikuwa akisubiri kufanyiwa upasuaji.

Kuhusu afya ya Mwamvita, Profesa Janabi alisema kwa sasa anaendelea vizuri na ameshapona tatizo linalomsumbua baada ya kufanyiwa upasuaji.

Mwamvita alifanyiwa upasuaji mkubwa wa kufungua kifua ambapo kwa sasa amepona na anatarajiwa kurudi nyumbani wakati wowote.