Achana na Ibrahim AjibMichaelruna Niyonzima. Achana na Joseph Omog na George Lwandamina. Achana na TFF na Bodi ya Ligi, njoo uwanjani.
Pamoja na mbwembwe, maneno, kejeli, tambo na yote ya aina hiyo, mwisho wa msimu bingwa wa Ligi Kuu Bara anatakiwa kuwa mmoja tu. Ni nani ataondoka na taji hilo lenye heshima zaidi katika soka la Tanzania? Kazi ipo.
Tathmini inaonyesha kwamba vita kubwa ya ubingwa itakuwa kwa timu nne tu kati ya 16 au 20 zitakazoshiriki. Timu nyingine zinategemewa kukamia mechi moja moja na kujiepusha na janga la kushuka daraja.
Timu kama Lipuli, Ndanda, Majimaji na Stand United, zinatazamiwa kuendelea kuwa wasindikizaji na kutumia muda mwingi katika eneo la chini badala ya kuwania ubingwa.
Timu za Mtibwa Sugar, Mbeya City na Mwadui zinatarajiwa kuwa katika eneo la katikati muda mwingi wa msimu huu, kutokana na kuwa na uwekezaji wa kawaida ambao hautoshi kuwasaidia kushinda ubingwa.
Timu zinazowania ubingwa sasa ni zipi? tunakuletea tathmini wakati huu ambapo pazia la Ligi Kuu linakwenda kufunguliwa kesho Jumamosi.
Simba 9/10
Tathmini mpaka sasa inaonyesha kwamba Simba ndiyo timu yenye nafasi kubwa zaidi ya kushinda taji la Ligi Kuu kwa msimu huu mpya.
Simba imesajili wachezaji 13 ambao ni makipa; Aishi Manula kutoka Azam, Said Mohammed ‘Nduda’ kutoka Mtibwa na Emmanuel Mseja kutoka Mbao FC. Timu hiyo imesajili pia mabeki; Yusuf Mlipili kutoka Toto Africans, Ally Shomary na Salim Mbonde kutoka Mtibwa.
Nyota wengine waliotua Msimbazi ni mabeki; Shomary Kapombe na Erasto Nyoni kutoka Azam na Jamal Mwambeleko kutoka Mbao FC. Pia kuna kiungo Haruna Niyonzima kutoka Yanga. Wengine ni washambuliaji John Bocco kutoka Azam, Emmanuel Okwi kutoka SC Villa ya Uganda na Nicholas Gyan kutoka Ghana.
Usajili wa Simba unaonekana kuwa na nguvu hasa katika nafasi ya ulinzi ambayo sasa itakuwa chini ya watu 12 wa nguvu, ambapo mabeki ni tisa na makipa ni watatu.
Eneo la kiungo nalo limeimarishwa kwa kuongezwa Niyonzima ambaye ametamba na Yanga kwa miaka sita na kushinda mataji tisa ya Ligi Kuu. Eneo hilo tayari lilikuwa na wakali kama Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na James Kotei.
Kwa namna ya upana wa kikosi cha Simba, ni wazi kwamba inaweza kupambana wakati wote wa Ligi na kushinda taji hilo.
Kitu kingine ambacho kinaipa nguvu ni uwezo mkubwa kifedha ambao inao kwa sasa ambapo mbali na kupata fedha za udhamini kutoka SportPesa, Vodacom na Azam TV, pia wanafadhiliwa na bilionea Mohammed Dewji.
Yanga 8.5/10
Mabingwa mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu Bara, Yanga, nao wana nafasi kubwa ya kutetea tena taji lao. Yanga bado ina kikosi imara cha kuweza kuwania taji hilo lakini italazimika kupambana na Simba imara.
Katika usajili wake, Yanga, imeimarisha maeneo yenye uhitaji maalumu kwenye kikosi chake ambapo imemsajili beki wa kati, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kutoka Zanzibar ili kuwaongezea nguvu Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani.
Timu hiyo imesajili pia viungo wawili wa shoka ambao ni Raphael Daudi kutoka Mbeya City na Kabamba Tshishimbi ‘Papii’ kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland huku pia ikiwaongeza Baruan Yahya na Ibrahim Ajibu kwenye safu yao ya ushambuliaji.
Pigo kubwa kwa Yanga ni kuondoka kwa winga wake tegemeo, Simon Msuva aliyejiunga na El Jadida ya Morocco. Msuva ameifungia Yanga mbaao 40 Ligi Kuu katika miaka mitatu iliyopita jambo ambalo linatosha kuonyesha umuhimu wake.
Nguvu kubwa ya Yanga itaendelea kuwa katika safu ya ushambuliaji chini ya kinara Amissi Tambwe ambaye atafanya kazi kwa ukaribu na Donald Ngoma na Obrey Chirwa.
Singida United 8/10
Timu hii inarejea Ligi Kuu baada ya muda mrefu, lakini tathmini inaonyesha kwamba ina nafasi pia ya kutwaa taji hilo. Baada ya Simba na Yanga, timu inayopewa nafasi kubwa ya kuondoka na taji hilo ni Singida United.
Timu hiyo imefanya usajili wa nyota zaidi ya 14 jambo linaloifanya kuwa na ushindani mkubwa. Miongoni mwa nyota makini ambao wamejiunga nao ni, Elisha Muroiwa na Muzdafa Kotinyu kutoka Zimbabwe pamoja na Danny Usengimana na Michael

EmoticonEmoticon