Real Madrid kawa mbabe wa Barcelona baada ya kumpiga ndani nje kwa jumla ya ambao 5-1 ikiwa mchezo wa awali weekend iliyopita Madrid ikifanya mauaji yakutisha kwa Barcelona jumla ya ambao 3-1 ambapo mchezo huo ronaldo akitokea bench na kuweka goli la pili na muda mchache kutolewa kwa kadi nyekundu lakini bado wakiwa pungufu madrid wakaweka la tatu katika dakika za nyongeza kupitia kwa Dogo kinda MARCO ASENSIO ambae kwa hivi sasa ndio habari ya mjini ndani ya mji wa real Madrid
Jana usiku ikiwa ni marudiano ya mchezo huo wa super cup bado madrid kaendeleza ubabe pasipo kuwepo kwa ronaldo Barcelona anakufa tena 2 mtungi ikiwa ni yuleyule kinda Dogo ambae ni habari ya mjini ambae mchezo uliopita alifunga mlango wa goli la mwisho leo amefungua mlango wa magoli ni dk ya 4 anapiga goli la umbali mrefu sana akiwashangaza watu wasiamini kilichotokea
Lakini kosakosa ziliendelea pande zote mbili lakini bado zimwi lililowatafuna Barcelona likaendelea ni pale benzema alipowaua Barcelona goli la pili dk ya 39 akiwaacha mabeki wa barcelona wakishangaa
Mchezo unamalizika real madrid 2 Barcelona 0 na kufanya jumla ya magoli kwa michezo yote miwili ni madrid 5 Barcelona 1
Hiyo madrid kawa bingwa wa super cup( mechi za ufunguzi wa ligi nchini hispania)
TAZAMA magoli ya jana hapa
EmoticonEmoticon