EMMANUEL MARTIN AJUMUISHWA TIMU YA TAIFA STARS KUCHUKUA NAFASI YA SIMON MSUVA
KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga Emmanuel Martin, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachojiandaa kuikabili Botswana, katika mcheo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa Jumamosi hii uwanja wa Uhuru.
Martin ambaye ni mara yake ya kwanza kuitwa timu ya taifa ya Tanzania Bara, alisema hakuamini pendi alipopataa taarifa hizo na anaamini huo ni mwanzo katika safari yake ya mafanikio katika soka.
“Namshukuru kocha kwa kuniona na kulipendekeza jina langu kuwa miongoni mwa wachezaji kwenye kikosi chake naamini nina kubwa ya kufanya ili kufikisha malengo ya timu,”alisema Martin.
Kiungo huyo alisema haikuwa rahisi kwani siku zote alikuwa akiwazia kuichezea timu ya taifa lakini hakupata bahati lakini nafurahi kuona ndoto zake zimetimia.
Amesema atahakikisha anaitumia vizuri nafasi hiyo aliyopewa ili kufanya vizuri na kujitengenezea uhakika wa kuwemo kwenye kikosi hicho kila kinapoitwa tena na kocha Salum Mayanga au yeyote atakayekuwepo.
Martin ameitwa kwenye kikosi cha Stars, kuziba pengo la Simon Msuva, ambaye uwezekano wa kuja kutoka Difaal El Jadida ya Morocco, umekuwa mdogo kutokana na viza yake kuisha muda na sasa uongozi wa timu hiyo upo kwenye mchakato wa kuhakikisha anapatiwa viza ya muda mrefu itakayomwezesha kuingia na kutoka nchini humo.
EmoticonEmoticon