Manchester United imetoa ofa ya paundi milioni 92 kwa ajili ya nyota wa Real Madrid Gareth Bale, kwa mujibu wa habari kutoka Hispania.
Chanzo cha Hispania, Don Balon kimedai kuwa Mashetani Wekundu wametoa dau hilo kwa ajili ya mchezaji wa Wales na miamba hao wa La Liga wanafikiria kukubali dili hilo.
Inadaiwa kuwa Real Madrid wanaamini ofa hiyo nono ya United ndiyo fursa ya kutengeneza faida kupitia Bale, ambaye walimsajili kutoka Tottenham kwa paundi milioni 86 miaka minne iliyopita.
Ripoti hiyo imeendelea kwa kusema kuwa Los Blancos hawawezi tena kumhakikishia Bale nafasi kikosi cha kwanza kutokana na kiwangocha Marco Asensio, jambo linaloweza kuharakisha biashara hiyo kuendelea.
Ikiwa uhamisho huo utafanikiwa, Bale atakuwa mchezaji wa tatu ghali zaidi katika ulimwengu wa soka,nyuma ya Neymar wa Paris Saint-Germain na Ousmane Dembele wa Barcelona.
EmoticonEmoticon