Thursday, August 31, 2017

MAJIBU YA KAMATI KUHUSU KESI YA CHIRWA NA KASEKE

Tags


Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la soka nchini (TFF) imetoa maamuzi ya kuwaruhusu wachezaji Deus Kaseke na Obrey Chirwa kuzitumikia timu zao baada ya kuwakosa na hatia katika tuhuma zilizokuwa zinawakabili.

Hata hivyo Kamati hiyo ilimpata na hatia Saimon Msuva ya kumuangusha mwamuzi wa mpambano wa mwisho la VPL kati ya Yanga dhidi ya Mbao FC.

Kamati imesema Msuva alitakiwa kufungiwa michezo mitatu pamoja na kupewa onyo kali.

Kamati itamwandikia barua la onyo Msuva kwa kuwa alishatumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu wakati wa mashindano ya SportPesa wakati huo akiwa bado ni mchezaji wa Yanga.




EmoticonEmoticon