Tuesday, August 29, 2017

TFF KUJADILI KESI YA CHIRWA NA KASEKE ALHAMISI HII

Tags


Kikao cha Kamati ya TFF ya saa 72 kinatarajiwa kufanyika Alhamisi ijayo ambapo mbali na mambo mengine kitajadili mashauri yanayowahusu wachezaji Obrey Chirwa na Deus Kaseke.

Chirwa ni wa yanga na kaseke kwa sasa yupo singida utd. Wote hawakucheza mechi za ligi iliyoanza weekend iliyopita hadi shauri lao litolewe maamuzi

Kaseke na Chirwa walisimamishwa kucheza baada ya kutuhumiwa kufanya fujo katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu msimu uliopita kati ya Yanga dhidi ya Mbao FC.

Ofisa Habari wa TFF alisema kikao hicho kitatoa uamuzi juu ya shauri hilo.

"Kikao kimechelewa kwa sababu ya uchaguzi na kubadilishwa kwa kamati za TFF, lakini mtakumbuka wachezaji hawa walisimamishwa kwenye mechi ya mwisho msimu uliopita,"alisema Lucas.


EmoticonEmoticon