Thursday, August 17, 2017

SIMBA SC LEO KUKIPIGA MECHI YA KIRAFIKI HUKO ZENJI

Tags


Mechi hii itakuwa LIVE MAJIRA YA SAA MBILI KAMILI USIKU AZAM SPORT 2


Klabu ya Simba leo tarehe 17 August 2017 itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege Fc ya Zanzibar katika Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar majira ya saa mbili usiku (20:00.) Mchezo huu utakuwa Live katika Kingamuzi cha Azam Tv Channel mpya ya Sports 2.

Ndugu msomaji wa MICHAKATOYETU Blog Klabu ya Simba imeweka kambi visiwani Zanzibar toka Jumatatu kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa Jadi Yanga Sc mchezo utakaochezwa Jumatano ya wiki Ijayo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.


Katika maandalizi hayo klabu ya Simba itajipima na Mlandege Fc klabu ambayo Jumapili iliyopita ilifungwa goli 2-0 na Yanga Sc katika Uwanja huo huo wa Amaan Mjini Zanzibar huku magoli ya Yanga yakifungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 50 na Emmanuel Martin dakika ya 73.

Ndugu msomaji wa MICHAKATOYETU Blog Mchezo wa leo dhidi ya Mlandege Fc utakuwa mchezo wa tano baada ya mwanzo kucheza minne miwili ya Afrika Kusini dhidi ya Orlando Pirates ambapo Simba ilifungwa goli 1-0 na mwingne dhidi ya Bidvest ambayo ilitoa sare ya goli 1-1 huko huko Afrika Kusini.

Baada ya kurudi Tanzania Simba ilicheza na Rayon Sports ya Rwanda ambapo Simba ilishinda kwa goli 1-0 na badae dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo pia ilishinda goli 1-0


EmoticonEmoticon