Thursday, August 17, 2017

JIFUNZE HAPA UMUHIMU WA KUMILIKI BIASHARA YAKO ILI UFANIKIWE

Tags


Huyu ni askofu GWAJIMA ambae kwa sasa ni kiongozi wa kidini anaetoa mafundisho mbalimbali kuhusu maisha kwa ujumla katika jamii katika nyanja ya kiroho, kiuchumi, kiafya na utamaduni.

Hapa utajifunza kidogo katika moja ya mafundisho yake kuhusu mafanikio ya maisha ya kila mmoja katika jamii zetu.


Nadhani hakuna asiependa kuona akisonga mbele na kufanikiwa katika maisha yake, lakini mafanikio yana mambo mengi sana ambapo ndani yake kuna michakato mingi.

Katika jamii kuna makundi mbalimbali ya watu wanaotafuta mafanikio


1. Waajiriwa
2.waliojiajiri
3.wafanyabiashara wakubwa
4.wawekezaji.

Ni vigumu sana kufikia mafanikio makubwa kama utakuwa kwenye kundi la namna moja na namba mbili

Kwanini, hizi ni sababu chache hapa chini


Kama umeajiriwa au umejiajiri ni vigumu sana kutoka kwani kama umeajiriwa inamaana kila kitu unapangiwa na utalipwa kulingana na boss wako alichokupangia hata kama utamzalishia asilimia mia moja yeye atakulipa kiduchu sana kwenye kile ulichazalisha ili uendelee kuwa tegemezi kwake daima, lakini pia hicho unachokifanya sio chako Bali ni cha mtu, vilevile kundi hili pia halina Uhuru wa muda ambapo unaweza kujiamulia nini tufanye saa ngapi na kipi usifanye Bali wewe muda wako inakuwa umenunuliwa na boss wako yeye ndio atapanga muda hivyo huwezi kwenda nje na muda Wa boss, lakini kundi hili kufanikiwa ni ngumu sana kwani unalipwa kutokana na nguvu yako pekee yako unayoifanya kwa boss wako na si vinginevyo, lakini pia kundi hili linakuhitaji lazima uwepo eneo la kazi ndipo uweze kupeleka mkono kinywani pale utakaposimama kufanya kazi siku hiyohiyo na kipato kinasimama.

Haya ni baadhi ya mambo yanayowabana kundi namba moja na namba mbili


KUNDI NAMBA TATU NA NAMBA NNE

Hawa ni wa chache sana lakini ni watu ambao wao wanatengeneza pesa hata wasipokuwepo eneo la tukio kwani wao wanachokifanya ni kuanzisha biashara ambayo utakuwa na misingi muhimu kama vile

1. Bidhaa/huduma
2.mfumo madhubuti wa kuendesha biashara hiyo
3.watu (timu)

Hivyo basi ili ufanikiwe lazima kwanza umiliki biashara yako ambayo utakuwa unabidhaa au kama sio bidhaa basi iwe ni huduma, na pia iwe na mfumo au system unaojiendesha na mwisho timu ya watu utakaoshirikiana nao kutengeza pesa hivyo Pato lako halitatokana na nguvu yako peke yako Bali litatokana na watu zaidi ya mmoja.

Mfano.

Wewe unaduka lako unafungua saa 1 asubuh na kugunga saa 11 jioni hapa unafanya kazi kwa masaa 10 kwa siku na unaingiza faida ya sh 5000 ndani ya saa 10. Kwa mwezi unatengeneza faida ya laki na nusu. Hii ni wewe peke yako


Lakini huwezi kumfikia mtu ambae yeye wanafanya kazi na timu. 

Mfano.
Tukulia MOHAMED DEWJI 

anatimu ya watu 500 wanafanya kazi kwa saa 10 kila mmoja anaingiza faida ya 5000 kwa siku anaingiza faida 5000×500=2500000. Kwa mwezi 2500000×30=75000000
Huo ni mfano tu wa mtu mwenye timu na asie na timu.

Hivyo basi ili ufanikiwe lazima ufanye kitu chenye mfumo huo ambao lazima uwe  na


1. Miliki biashara yako 
2. Iwe na mfumo madhubuti
3. Timu ya watu kuanzia watu 2 na kuendelea....

Hapa utahama kutoka kundi namba moja na mbili kwenda namba tatu na hatimae namba NNE.


Mfano wa watu wa chache walioko namba TATU NA NNE 

1.Mo

Ana biashara au kampuni yake inayotoa huduma na bidhaa

Ana mfumo unaojiendesha 

Ana timu ya watu 

Hivyo basi yupo kundi namba tatu na NNE.


2. Bakharesa

Ana kampuni au BIASHARA yake unaotoa bidhaa na huduma

Ana mfumo madhubuti (sytem)

Ana timu 

Wengine afrika ni

Dangote.

Duniani mfano

Biligate, trump

Wote wanamifumo hiyo mitatu.



Sasa unaweza kuona Hawa ni mbali na unaweza kusema ni vigumu kuwa kama wao hapana waochotuzidi hapo ni hivyo vitu vitatu.

Angalia hapo unapoishi wewe mtaani kwako wale unawaona wanamafanikio je pesa zao zinatokana na aina moja ya shughuli? Je anafanya kazi na watu wangap I kumtafuta pesa?. Jibu utakuta kwanza lazima anachokifanya ni chake mwenyewe na pia kina mfumo NA ana watu anafanya nao kazi na hata asipokuwepo bado anaingiza pesa.


MICHAKATOYETU BLOG inakuletea somo hili la namna ya kujifunza kufanya shughuli za ziada za kukuingizia kipato kwa muda wako wa ziada hata kama umeajiriwa au umejiajiri ambacho kina sifa zote tatu yaani biashara yako, yenye mfumo na yenye kuitumia timu.
Kujifunza somo hili kwa undani piga au follow whatsap 

0765503176


Msikilize askofu gwajima akitoa neno la UMUHIMU wa kufanya kitu chako ili ufanikiwe maana yeye pia amefanikiwa lakini anafanya kitu chake chenye kutoa huduma na chenye mfumo maalumu na chenye timu vilevile.











EmoticonEmoticon