Tuesday, August 8, 2017

UEFA SUPER CUP. MAN U KAFA ÑA MADRID KUWA BINGWA

Tags



MCHUANO wa Uefa Super Cup 2017 ambao uliwakutanisha klabu ya Manchester United dhidi ya Real Madrid ambao ni mabingwa wa klabu bingwa Ulaya ulimalizika na tukishuhudia Real Madrid waki isambaratisha United kwa mabao 2-1. Mchezo huo ulipigwa katika huko Skopje, Macedonia huku kukiwa na kiwango cha juu cha joto kali.


Madrid walidhibiti mchezo huo kuanzia kipenga cha kwanza kilichopulizwa.
Walijipata kifua mbele pale Casemiro alipowafungia, muda mfupi baada ya kugonga mwamba wa goli.
Waliongeza la pili kupitia Isco aliyefunga akiwa hatua nane kutoka kwenye goli baada ya kubadilishana pasi na Gareth Bale, ambaye alichezeshwa safu ya mashambulizi badala ya Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa United aliyenunuliwa kwa rekodo Romelu Lukaku alikomboa bao moja lakini Marcus Rashford akapoteza fursa nzuri ya kufunga kwa kuutuma mpira nje.
Real Madrid ndio timu ya kwanza kutetea Kombe la Super Cup la Uefa tangu 1990.
Mechi hiyo ilichezewa katika uwanja chini ya joto kali la nyuzi joto 30C katika mji mkuu huo wa Macedonia na ikawafanya wachezaji kupewa muda wa mapumziko mara mbili kupoesha joto, kama chini ya utaratibu wa Uefa.

Video fupi ya mchezo hii hapa



Like page yetu na share kwa magroup yote ya whatsap



EmoticonEmoticon