Wednesday, August 30, 2017

UTABIRI WA MSUVA KUHUSU BINGWA WA VODACOM MSIMU HUU

Tags

Simon Msuva ana amini kuwa klabu ya Yanga inayo nafasi ya kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo
Klabu ya Yanga itakuwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara nyingine tena kutokana wachezaji wengi kukaa kwa muda mrefu pamoja,  kadhalika na aina ya usajili bora walioufanya msimu huu kwa mujibu wa winga wazamani wa Yanga, Simon Msuva.
Msuva amejiunga na klabu ya Difaa el Jadida ya nchini Morocco, kwa dau linalokadiliwa dola 160,000 lilitumika kumg'oa Yanga.
“Nimefuatilia mechi za mwanzo za ligi ya Tanzania na nimesikia Simba wameanza kwa kushinda 7-0, wakati timu yangu ya zamani ya Yanga ikitoka sare, watu wengi wanasema Simba itakuwa bingwa, lakini binafsi naona Yanga ndiyo yenye nafasi ya kufanya hivyo tena.alisema hivyo wakati akihojiwa na mtandao wa Salehe Jembe.
“Nasema hivyo kwa sababu ukiangalia kweli zote zimefanya usajili wa maana, lakini Yanga ina wachezaji wengi waliokaa pamoja na kuzoeana tofauti na Simba yenye sura nyingi mpya.
Katuka hatua nyingine Msuva amehusifu usajili wa kiungo mkabaji wa Yanga raia wa Congo, Papy Tshishimbi kuwa ni ujio utakao leta tija sababu amekuja tatua tatizo la muda mrefu.
“Lakini pia, Donald Ngoma amerejea vizuri, na yule kiungo mkabaji waliyempata (Papy Tshishimbi), nadhani lile tatizo la siku nyingi limepata mtu sahihi wa kulitibu,” alisema Msuva.


EmoticonEmoticon