ULIZA UJIBIWE
HILI NI TAWI JIPYA LA MAJIMAJI FC LAFANYA SHEREHE YA UFUNGUZI LEO. 19/09/2017
leo ndani ya manispaa ya mjini Songea wale wapenzi na mashabiki wa majimaji wameungana na wenzao wanachama wa majimaji FC ambao wameunda TAWI jipya linaloitwa ULIZA UJIBIWE ambalo makao yake ni palepale uwanja wa majimaji nje kidogo na lango kuu la kuingilia uwanja wa majimaji
Sherehe hizo zimefanyika leo toka saa NNE asubuh hadi saa kumi jioni ikiwemo ni pamoja kutambulisha TAWI hilo lenye wanachama hai zaidi ya 138.
Sherehe hizo zimefanyika pamoja na wachezaji wote wa majimaji FC Wa msimu huu wa 2017/2018 na wageni wengine ni pamoja na wachezaji wa zamani wa majimaji walioichezea majimaji kwa mafanikio wakiwemo kina kabisama, betweli, MBOPA luoga ambae ndio alikuwa mgeni rasmi na pia ni mjumbe Mpya aliyechaguliwa kwa kura kwenye bodi ya majimaji chini ya mwenyekiti Mpya wa majimaji Mr Steven ngonyani alimaarufu SEVEN PHAMANCY.
Wachezaji wa majimaji wakisikiliza risala
Wageni waalikwa na wakiwa na wachezaji wa zamani wa majimaji FC wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mr MBOPA LUOGA
mjumbe Mpya wa bodi ya majimaji aliyepita kwa kuchaguliwa siku ya uchaguzi ambae alipata kura nyingi kuliko wajumbe wote kati ya wajumbe watano waliopita siku hiyo. Pia ni mchezaji wa zamani wa majimaji kwa miaka 20
Katika risala yao ya TAWI hilo jipya la ULIZA UJIBIWE, malengo yao ni kuipa support timu yao ya majimaji FC ndani na nje ya uwanja ikiwa ni pamoja kuhakikisha timu inapata mapato mazuri ili iweze kufanya vizuri, na kuhakikisha wanasafiri na timu ikiwa nje katika michezo yote ya majimaji FC.
Pia katika umoja huo wa TAWI wanamalengo ya kuwa na duka la TAWI, usafiri wao, ofisi na miundo mbinu yote itakayowezesha timu kupata manufa.
Shampeni ikifunguliwa na mmoja wa mwanatawi la Uliza Ujibiwe alimaarufu MPAMBALYOTO
Pia katika UFUNGUZI wa TAWI hilo leo kulikuwa na wawakilishi wa wadhamini wa majimaji FC wapya kutoka king'amuzi cha TING, ambao wao wanaanzisha MAJIMAJI TV itakayokuwa inarusha vipindi vya timu ya majimaji FC, muwakilishi huyo kutoka tingi (mjukuu wa Mzee MSEMWA ambae MSEMWA huyo ni alikuwa maarufu sana sana SONGEA) amesema watakuwa na majimaji kwa miaka 5 na kwa kuanzia wametenga muda wa masaa sita kwa ajili ya kurusha vipindi kuhusu majimaji na watakuwa wanarusha michezo ambayo majimaji anacheza.
Tawi la Uliza Ujibiwe baada ya kukata utepe
Pia ving'amuzi hivyo vitapatikana kwa ofa kwa wale wanachama hai wenye kadi kwa sh 100000 dishi na dikoda yake na baada ya hapo utalipia kwa bei ya ofa ya sh 15000 kwa mwezi na utapata kuona Chanel zaid ya 60/ikiwemo majimaji TV. Lakini ofa hii ni kwa wanachama wa majimaji wenye kadi. Hivyo ili upate ofa hii lazima ukachukue kadi ya majimaji kwanza katika ofisi za majimaji na ndipo utazipata ofa hizo za ving'amuzi palepale kwa viongoz wa majimaji na wao ndio watakaokuwa wanauza.
Baada ya ufunguzi huo wa tawi wageni na wachezaji wote walienda kupata chakula cha mchana.
Mwenye camera akionekana na tisheti ya njano ni mmoja wa wapiga picha kutoka kwa ving'amuzi vya TING akichukua baadhi ya matukio kwa ajili ya MAJIMAJI TV inayokwenda kupatikana kwenye ving'amuzi hicho.
Ni mimi niliyekuletea matukio yote ya sherehe hizi
Kutoka MICHAKATOYETU BLOG ambazo tulikuwa eneo la tukio LIVE
ENDELEA KUFUATILIA BLOG HII
KWA KIJIUNGA NA WHATSAP GROUP LA MICHAKATO YETU BLOG
Nicheki inbox 0765503176 kuweza kukuadd group la MICHAKATOYETU BLOG
LENYE KUKUPA MATUKIO YOTE KUHUSU MICHEZO NA MENGINE MENGI YA KIJAMIII
ASANTE NA.SHARE KWA WENGINE MAGROUP YAKO YOTE YA WHATSAP LINK HII
EmoticonEmoticon