Thursday, August 10, 2017

SINGIDA UTD SASA KUIVAA SIMBA.

Tags


Klabu ya Singida United imepata mwaliko wa mchezo wa kirafiki utakaofanyika uwanja wa taifa Dar es salaam.

Katika mchezo huo klabu ya Singida united itakakua mwenyeji huku ikiwakaribisha mabingwa wa Azam Sports Federation "Simba Sc".

Akiongea na kipindi cha michezo cha EFM mkurugenzi wa klabu hiyo Festo Sanga amesema Simba wajipange kwani klabu hiyo imejipanga na ikp vizuri katika kucheza kandanda safi huku akiahidi makubwa katika mchezo huo.

Alipoulizwa juu ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Yanga ,Sanga amesema: Yanga tulikua tunawafundisha namna mpira unavyochezwa. Alisema.


Hata hivyo Singida United ilipoteza mchezo wake wa awali wa kirafiki dhidi ya Yanga kwa goli 3-2.

Usisahau kushare 


EmoticonEmoticon